Encryption: Jinsi Inavyolinda Siri Zako Mtandaoni

Encryption ni Nini? | Jinsi Inavyolinda Data Binafsi๐Ÿ‘Œ

Fahamu jinsi encryption inavyofanya kazi, aina zake, na umuhimu wake katika kulinda siri zako mtandaoni dhidi ya wavamizi.


Encryption ni teknolojia ya kubadilisha taarifa zako kuwa msururu wa alama ambazo haziwezi kueleweka na yeyote isipokuwa mwenye ufunguo sahihi. Mfano wake ni ujumbe wa benki, barua pepe au mazungumzo ya mitandao ya kijamii. Bila encryption, taarifa zako zingekuwa rahisi kunaswa na wavamizi wa mtandao.

Kuna aina kuu mbili: encryption ya mwisho kwa mwisho (end-to-end) na encryption ya usafirishaji (in-transit). End-to-end inahakikisha ujumbe unasomwa na wewe na mlengwa pekee.

Kwa nini encryption ni muhimu? Husaidia kulinda data binafsi, kupunguza wizi wa taarifa za kifedha, na kuhakikisha faragha ya watumiaji. Makampuni makubwa hutumia teknolojia hii kwa sababu ni moja ya zana bora za data protection.

Hivyo basi, kila unapopokea ujumbe ulioandikwa “secured by encryption,” fahamu kuwa teknolojia hiyo ndiyo inakulinda dhidi ya macho ya wavamizi.

Mfano end to end  encryption kwa whatsapp ๐Ÿ‘‰ end to end encryption

Email:ayubu0208@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

usalama wa Nywila(password)

Linda Simu Yako kidigitali!

Siri za Kutengeneza Nywila Imara na Salama